Main Article Content

Abstract

Lugha ni nyenzo ya kipekee katika mawasiliano ya viumbe vyote. Kwa karne nyingi dhana
ya lugha imeibua mijadala mingi kiasi cha kuwafanya wanaisimu kubaki njia panda
kutokana na kukosa mwafaka kuhusu maana na chanzo cha lugha. Ingawa kuna imani
tofauti katika uso wa dunia hii, lakini imani zenye wafuasi wengi ni Ukristo na Uislamu.
Kwa mnasaba wa makala hii, mtazamo wa kiimani utakaorejelewa ni imani ya Kiislamu,
na hizo imani nyengine zitadokezwa tu itakapobidi. Mathalan, Usekula ni imani
isiyojinasibisha na maswala ya kidini katika maendeleo ya jamii kupitia nyanja zote za
kimaisha. Wasekula hawaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa ardhi na
mbingu na vyote vilivyomo ndani yake; akiwemo mwanadamu na lugha, bali huamini kuwa
vimetokea kwa bahati nasibu tu; na kwa hivyo vitatoweka pasi na utaratibu mahsusi.
Ukristo hueleza kuwa lugha ni zawadi kutoka kwa Mungu wa Adamu; ndiye aliyevipa vitu
vyote majina. Vivyo hivyo, unashikilia kuwa tofauti ya ndimi chanzo chake ni utengano
uliojitokeza baada ya mnara wa Babeli kuanguka na watu waliokuwa wanaupanda
kutapakaa sehemu mbalimbali. Uislamu ni dini inayoamini kwamba asili na chanzo cha
lugha ni Mwenyezi Mungu. Ni neema ya Mwenyezi Mungu1
kwa viumbe wake katika
mawasiliano ili wapate kulifikia vyema lengo la kuumbwa kwao. Kwa mantiki hiyo,
mjadala wa makala hii umeiangalia lugha kwa mtazamo wa Kiislamu kama
inavyoelezewa katika mafundisho yake,

Keywords

Mwenyezi Mungu MITAZAMO KISEKULA UCHANGANUZI

Article Details

Author Biography

Yasin Musa, Islamic university in uganda

Department of Literature, Language and Linguistics